Ijumaa 10 Oktoba 2025 - 18:21
Yemen Imezuia Bidhaa 560 Zinazohusiana na Kampuni za Kizayuni na Washirika Wake

Hawza/ Balozi wa Yemen Iran, akizingatia hatua za kuzuia bidhaa za Kizayuni, alisema kuwa: kama jibu kwa wito wa wananchi, serikali ya Yemen imezuia bidhaa 560 zinazohusiana na kampuni za Kizayuni na washirika wake.

Kwamujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, katika kikao cha pamoja kati ya Morteza Karamizian, Rais wa Shirika la Basiji la Vyombo vya Habari, na Mohammad Pourkhosh Saadat, Makamu wa Kimataifa wa Shirika la Basiji, na Ibrahim Al-Dailami, Balozi wa Jamhuri ya Yemen huko Tehran, pande zote  ziliweka mkazo katika ukuaji wa ushirikiano katika nyanja za vyombo vya habari, elimu, ujenzi, na muqawama.

Karamizian, katika mazungumzo hayo, alitoa shukrani zake kwa taifa la Yemen na kusema: “Ningependa kutoa pongezi kwa waandishi wa habari wa Yemen ambao wameuonesha ulimwenguni sura ya kikatili ya Kizayuni; ujasiri huu wa vyombo vya habari ni wa kupongezwa”.

Akibainisha jukumu la Basiji la Vyombo vya Habari, alisema kuwa hadi sasa Basiji imekusanya saini 2,000 kutoka kwa wanahabari kwa ajili ya kuunga mkono waandishi waliouawa Ghaza, na inafuatilia malalamiko rasmi dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Rais wa Shirika la Vyombo vya Habari la Basiji aliongeza kuwa, kwa kuwa Basiji ina makundi makubwa ya kijamii, ipo tayari kushirikiana na Yemen katika nyanja za kielimu, vyombo vya habari, na taaluma, na kutumia uwezo wa Basiji wa kisayansi katika kuendeleza miradi ya pamoja.

Mwisho wa mazungumzo, alisisitiza uthabiti wa mhimili wa muqawama na kusema: “Mustakbali ni ni wa miqawama, na mataifa huru yatafanikiwa katika mchakato huu”.

Aidha, Mohammad Pourkhosh Saadat, Makamu wa Kimataifa wa Shirika la Basiji, aliwashukuru wananchi wa Yemen kwa ushujaa wao katika kukabiliana na dhuluma, akasema: “Kwa niaba ya Basiji wa Iran, tunatoa heshima na shukrani kwa taifa na serikali ya kitaifa ya Yemen kwa kusimama dhidi ya ukatili. Tuko tayari kwa ushirikiano wowote na uhamishaji wa uzoefu katika nyanja za tiba, ujenzi, na vyombo vya habari”.

Aliongeza kuwa: “Leo vita vina matawi mawili; la kijeshi na la vyombo vya habari, na lazima tukabiliane na adui wa Kizayuni kwa njia bora katika pande zote mbili”.

Sehemu ya mwisho ya mazungumzo, Balozi wa Yemen aliushukuru ujumbe wa Iran na kushirikiana nao katika huzuni kutokana na mashahidi wa hivi karibuni wa serikali ya Yemen, akibainisha kuwa: “Maadui katika shambulio la hivi karibuni walikuwa na malengo matatu: kudhoofisha morali ya vyombo vya habari, kuidhoofisha serikali, na kutuzuia kuiunga mkono Ghaza, lakini hakufanikisha lolote kati ya hayo”.

Aliongeza kuwa baada ya kupata shahada watumishi wa serikali, hakukuwa na mzozo wa usalama, na wananchi walijumuika zaidi kuliko hapo awali. Taifa letu, licha ya changamoto za kiuchumi, limekusanya msaada wa kifedha na bidhaa kwa Ghaza, na kama jibu kwa wito wa wananchi, serikali imeizuia bidhaa 560 zinazohusiana na kampuni za Kizayuni na washirika wake.

Balozi wa Yemen pia alisema: “Vyombo vyetu vya habari viko katika mstari wa mbele wa kuendeleza muqawama; kwa upande mmoja vinaonesha sura ya kikatili ya Kizayuni, na kwa upande mwingine vinaakisi ujasiri wa taifa la Palestina na mhimili wa upinzani. Shughuli nyingi hizi ni za wananchi wenyewe na zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa”.

Al-Dailami, mwishoni mwa mkutano, aliashiria matumaini ya ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Basiji wa Yemen na Basiji wa Iran, huku akisema: “Tunatarajia kufaidika na uzoefu wa Iran, hasa katika nyanja za vyombo vya habari”.

Mwisho wa mazungumzo, pande zote mbili zilisisitiza katika ushirikiano wa vyombo vya habari, elimu, na utamaduni, na kuimarisha mhimili wa muqawama dhidi ya vita vya vyombo vya habari vinavyofanywa na adui.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha